Mshambuliaji wa klabu ya Dallas FC ya Marekani mwenye asili ya Tanzania Benard Kamungo amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Marekani kinachojiandaa kwaajili ya mashindano ya Olympic. Benard Kamungo aliwahi kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania lakini hakupata nafasi ya kuitumikia timu hiyo, mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, Oscar Mirambo amesema sababu ya kutokumtumia kwenye timu ya Taifa licha ya kujiunga na wenzake ni changamoto ya vibali kuchelewa.
Wakati tuna muita alikuwa na passport ya US lakini kwasababu alikuwa anahitaji kuitumikia timu ya Taifa na sisi tulikuwa tunamuhitaji tulimuita, baada ya mchakato tuliokuwa nao muda ulikuwa ni mfupi kwahivyo tulishindwa kumtumia kwenye mchezo ambao alitakiwa kucheza.
Mkurugenzi wa Ufundi TFF Oscar Mirambo akieleza sababu za kutokumtumia Kamugo Taifa Stars licha ya kujumuishwa kikosini.
Oscar Mirambo
Kwa upande mwingine Oscar amesema harakati za kuhakikisha Benard Kamugo anaitumikia Tanzania kwenye michuano mbalimbali bado zinaendelea kwani hata kama atacheza timu ya Taifa ya Marekani chini ya miaka 23 kwenye michuano ya Olympic atakuwa bado na nafasi ya kuitumikia timu ya wakubwa ya Tanzania kama ambavyo baadhi ya wachezaji nyota waliwahi kufanya.
Harakati za kwetu bado zinaendelea, kusikia kwamba ameitwa kwenye timu inayoenda kwenye Olympic ni habari kama habari nyingine kwa maana ndani ya ofisi michakato ilikuwa bado inaendelea kwahiyo tunasubiri kupata maamuzi yake ya mwisho yatakuwaje.
Oscar Mirambo akizungumza kuhusu uwezekano wa Kamugo kuitumikia Taifa Stars.
Benard Kamugo alipoitwa timu Taifa ya Tanzania.
Kuhusu wachezaji wengine wenye asili ya Tanzania wanaocheza nje ya Tanzania mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la Soka Tanzania Oscar Mirambo amesema kwakuwa ni jambo la nchi vyombo vya nchi ndio wanafanya kazi hiyo tayari wamewasilisha taarifa zao na hivi karibuni mafaili yatarudi ofisini kwao.