NBC Premier League

MWENENDO WA NPL HADI MZUNGUKO WA TANO.

Klabu ya Simba inashikilia rekodi ya kucheza michezo mitano mfululizo ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara bila kupoteza kwa msimu huu wa 2023/24.

Published on

Ligi kuu kandanda Tanzania Bara msimu wa 2023/24 kwasasa ipo kwenye mapumziko kupisha michezo ya kimataifa ya Timu za Taifa iliyo kwenye Kalenda ya FIFA. Ligi hiyo imesimama baada ya mzunguko wa Tano kutamatika kwa kila timu kucheza michezo mitano (5) na hiya ndio yaliyotokea;

Hadi hivi sasa klabu za Simba na Azam ndizo hazijapoteza mchezo katika michezo mitano zilizocheza, Simba imevuna alama zote kumi na tano (15) wakiwa na wastani wa asilimia 100 za ushindi, hii inakuwa timu ya kwanza kwa msimu wa 2023/24 kushinda mechi tano (5) mfululizo na Azam wameshinda michezo minne (4) na kutoa sare mchezo mmoja (1) wakivuna alama kumi na tatu (13).

Hadi hivi sasa klabu za Namungo, Mtibwa Sugar na Coastal Union ndizo hazijaonja radha ya ushindi. Namungo chini ya kocha Cedric Kaze wameambulia sare tatu (3) pekee na kupoteza michezo miwili (2) wakiwa na Alama tatu (3) katika nafasi ya 14 ya msimamo wa Ligi. Mtibwa Sugar wao wametoa sare michezo miwili (2) na kupoteza michezo mitatu (3) wakivuna alama mbili (2) wakiwa katika nafasi ya 15. Coastal Union iliyochini ya kocha mwinyi zahera nao wamepoteza michezo mitatu (3) na kutoa sare mbili (2) wakivuna alama mbili (2) katika nafasi ya 16.

Vinara wa mabao hadi kufikia hivi sasa ni Jean Baleke [Simba] (5), Feisal Salumu [Azam] (4), Pacome Zouzoua [Yanga] (3), Ki Aziz [Yanga] (3), Max Nzengeli [Yanga] (3) na Matheo Anthony [Mashujaa] (3). Kinara wa upigaji pasi za mwisho (Assist) ni Kouassi Yao [Yanga] (3).

Goli la mapema zaidi msimu huu limefungwa na Yassin Mgaza wa Dodoma Jiji dakika ya kwanza (1) walipokuwa wanacheza dhidi ya Tabora United, wengine waliofuatia ni Pacome Zouzoua wa Yanga dakika ya tatu (3) dhidi ya Ihefu, Feisal Salum wa azam fc dhidi ya Tabora United dakika ya tatu (3).

Magolikipa vinara wa hati safi (Cleansheet) hadi hivi sasa ni Idrisu Abdulai [Azam] (3), Djigui Diarra [Yanga] (3).

Popular Posts

Exit mobile version