Simba

SIMBA YAENDELEA KUJIANDAA NA AL AHLY.

Klabu ya Simba imeendelea na maandalizi yake kuelekea mchezo wa ufunguzi wa michuano ya African Football League.

Published on

Klabu ya Simba katika kipindi hiki cha mapumziko ya kupisha michezo ya timu za Taifa, imeendelea na maandalizi yake kuelekea mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya African Football League dhidi ya Al Ahly utakaopigwa October 20, katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.

Simba leo asubuhi imecheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya klabu ya Dar city inayoshiriki Ligi daraja la kwanza na kuibuka na ushindi wa goli 5-1, magoli kwa upande wa Simba yakifungwa na Shaban Chilunda akiingia kambani mara mbili (2), Luis Miqquisone aliyeingia kambani mara moja (1), Onana akifunga moja (1) na Said Ntibazinkiza aliyefunga goli moja (1).

Popular Posts

Exit mobile version