Taifa Stars

TAIFA STARS YATOSHANA NGUVU NA SUDAN.

Taifa Stars imetoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan uliofanyika Saudi Arabia.

Published on

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars hii leo imecheza mchezo wa kirafiki Ugenini dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan huko nchini Saudi Arabia na mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1 magoli yaliyofungwa kipindi cha kwanza cha mchezo.

Timu ya Taifa ya Sudan ilianza kupata goli mapema kupitia kwa mshambuliaji wa Al Hilal Musab Ahmed aliyepachika dakika ya 15 ya mchezo kabla ya Taifa Stars kusawazisha kupitia kwa kiungo wa klabu ya Azam Israel Sospeter Bajana mnamo dakika ya 40 ya mchezo.

Popular Posts

Exit mobile version