Klabu ya Ihefu Sc imemtangaza Moses Basena raia wa Uganda kuwa kocha wao Mkuu akirithi nafasi ya Zubeir Katwila.
Basena aliwahi kufanya kazi kama kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Uganda, lakini pia amefundisha vilabu vya URA FC na SC Villa.
Utambulisho wa kocha Basena umekuja baada ya siku mbili kupita tangu klabu ya Ihefu ivunje mkataba kwa makubaliano ya pande zote mbili na aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Zubeir Katwila.
Mara baada ya Moses Basena kuteuliwa kuwa kocha mkuu, ataiongoza klabu ya Ihefu katika michezo mbalimbali ya ligi kuu ya NBC na ile ya kombe la Shirikisho la Azam {ASFC}