Nyota wa zamani wa klabu ya PSG, Barcelona,Manchester United, AC Milan na klabu kadhaa Barani Ulaya Zlatan Ibrahimovic amesema tangu alipoondoka Ligi kuu soka nchini Marekani (MLS) Ligi hiyo iliishiwa mashabiki kwani asilimia kubwa walihamia kufuatilia mchezo wa Baseball lakini kwasasa ujio wa Messi ndani ya Inter Miami umewafanya mashabiki kuanza kufuatilia tena Ligi ya MLS.
Ninafurahi kwaajili yao, wanaweza kuangalia mpira tena, nilipoondoka walianza kuangalia mchezo wa Baseball.
Zlatan Ibrahimovic akizungumza kuhusu messi kujiunga na MLS.
Nyota huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic alijiunga na LA Galaxy mwaka 2018 hadi 2019 na akafunga magoli 53 katika michezo 58 aliyoitumikia klabu hiyo.