Klabu CR Belouizdad ya nchini Algeria imemtangaza Kocha Marcos Paqueta raia wa Brazil kuwa kocha wao Mkuu akichukua nafasi ya Sven Vandenbroecks waliyeachana nae
Belouizdad imechukua uamuzi huo baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wao Sven Vandenbroecks kwa sababu ya kukiuka kanuni za mkataba wake namna ya uendeshaji wa timu hiyo na kupelekea uongozi wa Klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake bwana Mahdi Rabh kuchukua jukumu la kuvunja mkataba nae wiki mbili zilizopita
Marco Paquieta(65) amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana ya Brazil, Klabu ya Botofogo ya Brazil, lakini pia ana uzoefu na Soka la Afrika kwani amewahi kufanyakazi katika klabu kubwa kama vile Zamalek ya Misri pamoja Hassania Agadir ya Morocco na pia aliwahi kuifundisha CR Belouizdad msimu wa 2021/22
Itakumbukwa kwamba CR Belouizdad, imepangwa kundi moja na Klabu ya Yanga ya Tanzania ?? kwenye michuano hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika.