Kocha wa zamani wa klabu ya Simba Pablo Franco Martin ambaye kwasasa anafundisha klabu ya Amazulu inayoshiriki Ligi kuu kandanda nchini Afrika Kusini amewafungia kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza nyota watatu wa klabu ya Amazulu na sasa wanafanya mazoezi na kikosi cha pili cha klabu hiyo. Nyota hao ni Mswati Mavuso, Mxolisi Kunene na Sphesihle Maduna kwa sababu mbalimbali.
Taarifa kutoka kwenye chanzo cha karibu cha mchezaji Sphesihle Maduna zinasema kuwa chanzo cha nyota huyo kuondolewa kwenye kikosi cha kwanza ni kukataa kuongeza mkataba mpya na kikosi cha AmaZulu ambapo mkataba wake wa awali unamalizika mwezi wa sita mwaka ujao, huku akisisitiza kuwa anahitaji kujiunga na Kaizer Chiefs.
Maduna alipewa mkataba mpya na Amazulu lakini aliukataa, ndoto yake ni kujiunga na Kaizer Chiefs, mkataba wake wa mwisho na AmaZulu utaisha mwezi wa sita mwakani, hivyo yupo huru kusaini mkataba wa awali na klabu yoyote mwezi Januari.