Timu ya Taifa ya Zimbabwe inampango wa kucheza nchini Rwanda mchezo wake wa nyumbani dhidi ya Nigeria wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la Dunia 2026. Hii inakuja baada ya shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) kusema viwanja vilivyopo havikidhi vigezo vya kuchezewa michezo ya kimataifa.
Timu ya Taifa ya Zimbabwe imepangwa kucheza mchezo wake wa kwanza ugenini dhidi ya Rwanda na baada ya siku nne itacheza mchezo wa pili ikiwa mwenyeji dhidi ya Nigeria mchezo ambao wanapanga kuucheza nchini Rwanda ili kuepusha gharama sa kwenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini.
Kulingana na ripoti ya ZimLive shirikisho la soka nchini Zimbabwe (ZIFA) na shirikisho la soka nchini Rwanda wapo kwenye mazungumzo kuhusiana na timu hiyo kucheza mchezo wao dhidi ya Nigeria nchini Rwanda.
Mbunge wa Mt. Pleasant Fadzayi Mahere kutoka chama cha upinzani cha Coalition for Change aliulizia kuhusiana na ukimya wa Waziri wa Michezo Kirsty Coventry nchi kama Zimbabwe inayofahamika kwa kuwa na wapenzi wengi wa mpira haina uwanja unaokidhi kwa michezo ya kimataifa.
Miaka 43 tangu tumepata uhuru, hatuna hata uwanja mmoja unakidhi vigezo vya kuchezea mchezo wa kimataifa?. Sasa tunakutana na aibu ya kucheza mchezo wetu wa nyumbani Kigali, hii inatoa hamasa gani kwa wachezaji wetu?, mashabiki wataiangaliaje timu yai ?,
Mbunge Mahere aliuliza.
Timu zingine zilizo kundi C pamoja na Zimbabwe ni South Africa, Lesotho na Benin.