Makala Nyingine

SANE KUWA MBADALA WA MO SALAH LIVERPOOL.

Klabu ya Liverpool ina mpango wa kumsajili Leroy Sane kama mbadala wa Mo Salah endapo atatimka kikosini hapo.

Published on

Klabu ya Liverpool inatajwa kuihitaji saini ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na timu ya Taifa ya Ujerumani Leroy Sane kuwa mbadala wa Mohamed Salah endapo ataondoka klabuni hapo majira ya kiangazi msimu ujao. kipindi cha Kiangazi kilichopita klabu ya Al Ettihad inayoshiriki Ligi kuu nchini Saudi Arabia ilihitaji kuipata saina ya nyota huyo wa timu ya Taifa ya Misri Mohamed Salah.

Mohamed Salah (31) amebakiza mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia Liverpool na kuna uwezekano mkubwa wa nyota huyo kuondoka msimu ujao akiwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja. Sane aliwahi kucheza nchini England akiwa na kikosi cha Manchester City na ana historia ya kuifunga Liverpool mara nne mfululizo huku kumbukumbu kubwa ikiwa msimu wa 2018/19.

Popular Posts

Exit mobile version