Mchezaji wa klabu ya Manchester City Kalvin Phillips anaweza kuondoka Januari kwa sababu anataka kupata muda zaidi wa kucheza.
Nikiwa kama mchezaji wa mpira wa miguu, nataka kucheza kila wakati, na hivyo ndivyo ninataka iwe, ni wazi kwamba ninahitaji dakika nyingi zaidi za kucheza
Alisema Kalvin Philips ambaye ni mchezaji wa klabu ya Manchester City
Sijafanya hivyo kwenye kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita, kwa hiyo hilo ni jambo moja ninalotaka kulifanya pia kwenye michuano ya Euro
Kalvin Philips aliendelea kusisitiza
Kauli hiyo inaonesha kwamba kiungo huyo Muingereza yuko tayari kuondoka katika viunga vya Etihad kwenda kutafuta changamoto mpya kwingineko ambako atapata muda mwingi kukitumikia kipaji chake
Dirisha la Januari? Ngoja tuone kitakachotokea.
Kalvin Philips alijibu swali kuhusiana na uwezekano wa kuondoka katika kikosi cha Manchester City
Ikumbukwe kuwa Kalvin Philips alijiunga na kikosi cha Manchester City kutoka Leeds United mwaka 2022 kwa ada ya uhamisho £45m, huku tangu ajiunge na wababe hao ameshindwa kupenya katika kikosi cha kwanza cha Pep Guardiola kutokana na majeraha ya mara kwa mara na ushindani mkubwa wa namba katika nafasi anayocheza