International Football

SIR RATCLIFFE ATAKA UTAWALA WA MASUALA YOTE YA SOKA UNITED

Published on

Wakati bodi ya Manchester United inatarajia kukaa kesho, Alhamisi, kupiga kura juu ya kuuziwa aslimia 25 za hisa ndani ya United kwa kiasi si chini ya Pauni bilioni 1.5 kwa Bilionea Sir Jim Ratcliffe wa Uingereza, amesema kuwa atakapokuwa kama mmiliki mpya atataka usimamizi wa masula yote yanayohusiana na soka ndani ya klabu ikiwemo sajili, wakurugenzi wa michezo na benchi la ufundi.

Ratcliffe, ambaye anabaki kuwa mnunuzi pekee baada ya Sheikh Jassim wa Qatar kujitoa kwenye kinyang’anyiro mapema Jumamosi, anaamini kuwa namna pekee ya kurejesha imani kwa mashabiki wa United ni kuhakikisha zinafanyika sajili za maana na kuirejesha timu kwenye makali yake yaliyozoeleka na hili linawezekana akipata usimamizi kamili wa mambo yote hayo.

Itakumbukwa kuwa mwezi Machi mwaka huu, bilionea huyo alikosoa sajili za United za hivi karibuni kuwa sio zenye malengo ya baadae huku akitolea mfano wa usajili wa Casemiro aliyesajiliwa kutoka Real Madrid kwa euro milioni 60 akiwa tayari na miaka 30 na kupewa mkataba mkubwa wa miaka minne na mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki.

Nice ya ufaransa ambayo pia ni timu anayoimiliki, iliwasajili Kasper Schmeichel kwa pauni milioni 1 huku Ross Barkley na Aaron Ramsey wakisajiliwa bure na wote kwa mwaka mmoja pekee walipomaliza wakaachwa kutokana na kigezo alichokisema cha umri, hivyo hakuona sababu ya mchezaji wa miaka 30 kusajiliwa kwa gharama zote zile, akimmzungumzia Casemiro ambaye alikuwa na msimu mzuri uliopita lakini msimu huu bado anajitafuta.

Mengi yanasemwa juu ya umiliki wa Ratcliffe huku wengi wakihoji kuendelea kuwepo klabuni kwa CEO wa klabu Richard Arnold na Mkurugenzi wa michezo John Murtough ambao hasa wanahusika na vitengo vya usajili pindi atakapoidhinishwa na bodi ya klabu kuwa mmiliki mpya mwenye hisa robo ya klabu.

Popular Posts

Exit mobile version