Wakala wa nyota wa timu ya Taifa ya Ghana na klabu ya Westham United Mohamed Kudus, Jen Mendelewitsch amesema kuwa klabu ya Chelsea ilikuwa miongoni mwa klabu nyingi zilizopeleka ofa kwenye klabu ya Ajax kwaajili ya kuinasa saini ya Mohamed Kudus, lakini ofa yao ilikuwa ndogo hivyo Ajax wakaikataa ofa hiyo.
Jen anasema klabu ya Chelsea na mchezaji walikuwa tayari wamekubaliana kila kitu lakini Ajax wakaipiga chini ofa ya £17 million wakisema ni kiwango kidogo ambacho hakiendani na uwezo wa mchezaji huo
Mendelewitsch anasema Chelsea walikuwa wanatumia mbinu za kukubaliana na wachezaji kisha wanatoa kiwango kidogo kwa klabu inayommiliki mchezaji, inaaminika klabu hiyo iliamua kuwekeza nguvu nyingi katika usajili wa kiungo kutoka Brighton Moises Caicedo.
Tulifikia makubaliano na Chelsea, na tulifikia makubaliano ya kusaini mkataba lakini hatukusaini. Aliongea na kocha, lakini mwisho wa siku hakuna kilichotokea kwasababu Chelsea walitoa ofa ndogo kwa Ajax, Chelsea imefanya hivyo kwa klabu nyingi sana msimu huu, wanatoa ofa ndogo huku wakijua kabisa klabu haitakubali lakini ukweli ni kwamba waliwekeza nguvu nyingi kwenye usajili wa Caicedo.
Jen Mendelewitsch akizungumzia kilichotokea.
Kabla ya kujiunga na klabu ya Westham kwa dau la £38m pia klabu ya PSG ilikuwa miongoni mwa timu zilizopewa kipaumbele cha kumsajili kabla klabu hiyo haijajitoa kwenye usajili huo.
Tulipeleka wasifu wake kwenye klabu ya PSG, lakini ulikuwa ni uamuzi wa klabu kuamua kujitoa kumsajili. Kila klabu ina haki ya kuamua mchezaji gani imsajili.
Jen Mendelewitsch alisema kuhusu Kudus kuhitajika na PSG.