Kocha wa zamani wa klabu ya Simba na klabu kadhaa hapa nchini Jamhuri Kihwelu “Julio”, amesema katika kipindi kama hiki kuelekea mchezo mkubwa kama wa Simba na Al Ahly makocha wanajitahidi sana kuwambia wachezaji wacheze kwa tahadhari huku wakijua wanacheza na mpinzani mwenye uwezo mkubwa na pindi wanapopata nafasi waweze kuzitumia.
Mara nyingi huwa tunawaambia wachezaji wetu kucheza kwa tahadhari, kujua kwamba unacheza na mpinzani wa aina gani, kwa hiyo unavyojua unacheza na mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko wewe lazima ucheze kwa tahadhari na mnapopata nafasi wachezaji watulie na kuzitumia. Kwasababu tunacheza na timu ambayo ina ukubwa zaidi basi inatakiwa kucheza kwa tahadhari.
Jamhuri Kihwelu.
Jamhuri Kihwelu amesema ufunguzi wa mashindano ya African Football League utaongeza chachu na hamasa kwa wachezaji vijana ili wapambane zaidi nao siku moja wapate nafasi ya kushiriki au kuwa sehemu ya historia kama ambavyo Simba wanaenda kufanya.
Vijana wanatakiwa nao wakazane ili waendelee kupata nafasi ya kuja kucheza mashindano haya, ambayo yakiwa hapa nyumbani au mahala pengine popote au kujitangaza na kuweza kutoka nje ya nchi.
Jamhuri Kihwelu juu ya faida inayopatikana kwenye soka letu kutokana na ufunguzi kufanyika Tanzania.
Klabu ya Simba itacheza mchezo wa ufunguzi wa michuano mipya ya African Football League dhidi ya Al Ahly katika dimba la Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam, kesho October 20, saa 06:00 Jioni.