Shirikisho la soka Barani Asia limekataa ombi la shirikisho la soka nchini Palestina kuhusu michezo yake kufanyika nchini Algeria, awali Shirikisho la soka nchi Palestina liliomba litumie nchi ya Algeria kama mwenyeji wa michezo yake kutokana na kile kinachoendelea nchini mwao.
Algeria imeonyesha kuwa pamoja na nchi ya Palestina. Siku mbili zilizopita shirikisho la soka nchini Algeria lilitangaza kusitisha shughuli zote za michezo nchini humo, hadi pale watakapotangaza kurejesha tena kutokana na kile kinachoendelea nchini Palestina.
Waziri wa vijana na michezo nchini Tunisia, Kamal Daqish hivi karibuni pia alitangaza kuwapa nguvu wachezaji wote wenye uraia wa Tunisia, ambao wanatishiwa na klabu zao kutokana na kuumizwa na kile kinachoendelea katika ukanda wa Gaza.
Makamu wa tatu wa Rais wa Shirikisho la soka Barani Afrika kutoka Djibout Waberi Souleiman amekuwa mjumbe wa kwanza wa kamati kuu kusimama na nchi ya Palestina.