Klabu ya Ihefu kutoka mkoani Mbeya imeendelea kuliboresha benchi lake la ufundi kwa kumuongeza raia wa Uganda Fred Kisitu Kajoba kuwa kocha wa magoli kipa.
Wasifu wa Fred Kisitu Kajoba unaonesha kuwa amewahi kuzifundisha timu za Vipers Sc, Uganda Queens na timu ya Taifa ya Uganda “The Cranes” akiwa kocha wa Magolikipa.
Kocha Fred Kisitu Kajoba anakwenda kuongeza nguvu katika benchi la ufundi la timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya NBC baada ya siku tatu tu kupita tangu timu hiyo kufikia makubaliano na kumtangaza kocha mkuu raia wa Uganda Moses Basena, aliyechukua nafasi ya Zubeir Katwila waliyevunja nae mkataba kwa makubaliano ya pande zote mbili wiki moja iliyopita.