Shirikisho la soka Barani Ulaya UEFA limesema mchezo ulioahirishwa Jumatatu, October 16 kati ya Belgium na Sweden hautarudiwa na matokeo yataendelea kusalia kama yalivyo (1-1). Mchezo huo ulilazimika kuahirishwa kipindi cha pili baada ya tukio la mashabiki wawili waliokuwa wamevalia jezi za timu ya Taifa ya Sweden kupigwa risasi nje ya dimba la King Baudouin, Jijini la Brussels.
Mchezo huo ulikuwa ni wa kundi F wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya Euro 2024 itakayofanyika nchini Gerany. Belgium inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 17, 2. Austria 16, 3. Sweden alama 7, 4. Azerbaijan alama 4, 5. Estonia alama 1.