Shirikisho la soka Barani Afrika leo limeutangaza mpira wa MACRON Earthquake XH kuwa mpira rasmi utakaotumika katika mashindano ya African Football League msimu huu. Gharama ya mpira huu ni Euro 102.50 (TZS 271,762.38).
Mipira yote ya MACRON inatengenezwa chini ya uangalizi wa shirikisho la soka Duniani FIFA. Mpira huu una ubora wa kutosha kutumika kwenye mashindano mbalimbali kwani umekaguliwa kipimo chake, uzito, unavyodunda na mzunguko wake na maabara yenye ubora mkubwa.
Michuano hii itaanza rasmi leo katika dimba la Benjamin Mkapa kwa mchezo wa ufunguzi kati ya Simba na Al Ahly saa kumi na mbili Jioni. Michuano hii inashirikisha timu nane pekee kutoka pande zote za Afrika.