International Football

TAKWIMU ZA TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA ZINATISHA

Published on

Takwimu za timu ya Taifa ya Argentina ambao ndio washindi wa Kombe la Dunia la 2022 zinaogopesha kwani mpaka sasa wamecheza jumla ya mechi 51 katika mashindano rasmi yanayo simamiwa na Shirikisho la mpira duniani FIFA, wakiwa hawajapoteza jumla ya michezo 50.

Sambamba na hilo safu ya ulinzi ya timu hiyo inayoongozwa na golikipa Emiliano Martínez ‘Dibu’ imekuwa na muendelezo wa kiwango bora kwani haijaruhusu bao kwenye dakika 712 mfululizo sawa na miezi kumi (10).

Nahodha wa timu hiyo Lionel Messi akiwa ndiye kinara wa upatikanaji wa mabao, akiwa amehusika kwenye jumla ya mabao 53, ikiwa ni magoli pamoja na usaidizi wa pasi za mabao katika michezo aliyoichezea timu yake ya Taifa. Huku timu hiyo ya Taifa ikiwa imefunga jumla ya mabao 39 na pasi za usaidizi wa mabao 14.

Popular Posts

Exit mobile version