Makala Nyingine

FT: PETRO ATLETICO 0-2 MAMELODI SUNDOWNS (AFL).

Mchezo wa African Football League kati ya Petro Atletico de Luanda dhidi ya Mamelodi Sundowns unaendelea.

Published on

MWENENDO WA MCHEZO PETRO ATLETICO VS MAMELODI SUNDOWNS

Mchezo Umeanza.

Dakika ya 7′

Mchezaji wa Petro Atletico Alexandre Guedes anapata nafasi ya wazi baada ya mabeki wa mamelodi Sundowns kujichanganya wakati wakiondoa mpira langoni mwao na anaokoa golikipa wa Mamelodi Sundowns Ronwen Williams.

Dakika ya 12′

Mlinzi wa klabu ya Mamelod Sundowns anapata kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Gilberto mshambuliaji wa klabu ya Petro Atletico.

Dakika 15′

Mwenyeji wa mchezo Petro Atletico ameutawala mchezo, amefika mara nyingi zaidi langoni mwa Mamelod Sundowns.

Dakika ya 20′

Matokeo, Petro Atletico 0-0 mamelodi Sundowns.

Dakika ya 25′

Gilberto anapiga pasi ya chini chini kutokea kulia mwa uwanja na kumkuta Eddie Guedes anayeunganisha kwa Toro aliyepiga moja kwa moja na golikopa wa Mamelod Sundowns Ronwen anaiweka timu yake salama kwa kuokoa mchomo.

Dakika ya 30,

Kiungo wa Atletico Petro Carlinhos anapiga kona lakini Gilberto anapiga kichwa kinachoelekea nje ya lango.

Dakika ya 32

Mchezaji wa Atletico Gilberto anaupata mpira kutoka kwa Marco Allende wa Mamelodi Sundowns aliyeteleza na kudondoka chini kisha Gilberto anampa pasi Toro ambaye anapiga nje.

Dakika ya 35,

Marco Allende wa Mamelodi anapiga pasi mpenyezo kuelekea kwa Zwane ambaye anapiga moja kwa moja Dakika nje ya lango.

Dakika ya 38,

Petro Atletico wanapata Penalty baada ya Jonathan Toro kuangushwa ndani ya kisanduku cha 18 na beki wa Mamelodi Sundowns Mothobi Mvala.

Dakika ya 41 ,

Golikipa wa Mamelodi Sundowns Ronwen Williams anaokoa Penati ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya Petro Atletico Golberto Jezi namba 27. Ronwen anapangua shuti kali la Guedes.

Dakika ya 45,

Mamelodi Sundowns wanapata kona inayoondoshwa vyema na Miguel beki wa Petro Atletico.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika suluhu ya 0-0.

Dakika ya 46.

Kiungo wa Mamelodi Sundowns Teboho Mokoena anamfanyia madhambi kiungi mshambuliaji wa Petro Atletico Anderson Cruz.

Dakika ya 50,

Mechi bado ngumu matokeo 0-0.

Dakika ya 53,

Teboho Mokoena anapiga shuti kali langoni mwa Petro Atletico na anauondoa kimaridadi sana mlinda lango wa Petro Atletico Hugo Marques.

Dakika ya 58,

Shuti la Aubrey Modiba linaokolewa na golikipa wa Petro Atletico Hugo Marques na kuiweka timu yake salama.

Dakika ya 63,

Petro Atletico wanafanya mabadiliko, anakwenda benchi jezi namba 7 Anderson Cruz anaingia Augusto Carneiro jezi namba 13. Anatoka Alexandre Guedes jezi namba 23 anaingia Alexandre Domingos Ngunza Caculo jezi namba 36.

Dakika ya 68,

Mamelodi wamepata goli kupitia kwa Marcelo Allende baada ya kupokea pasi ya mpenyezo kutoka kwa Junior Mendieta, baada ya gonga gonga safi ya wachezaji wa Mamelodi Sundowns.

Dakika ya 72,

Petro Atletico 0-1 Mamelodi Sundowns.

Dakika ya 74,

Mamelodi Sundowns wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili. Anatoka Jezi namba 20, Jonathan Toro anaingia jezi namba 11, Jaredi Lopes Teixeira, anatoka jezi namba 25, Eddie Afonso, anaingia jezi namba 19, Erivaldo.

Dakika ya 78,

Petro Atletico de Luanda 0-1 Mamelodi Sundowns.

Dakika ya 79,

Mamelodi Sundowns wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili, jezi namba 18 Teboho Zwane anaingia Gaston Sirino, anatoka jezi namba 15, Junior Mendieta, anaingia jezi namba 33 Thapelo Maseko.

Dakika ya 81,

Thapelo Maseko anaiandikia goli la pili Mamelodi Sundowns.

Dakika ya 85,

Golikipa wa Mamelodi Sundowns Ronwen Williams anaiokoa timu yake baada ya kuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na mshambuliaji wa Petro Atletico de Luanda Tiago Azulao jezi namba 26 aliyeingia kuchukua nafasi ya Jonathan Toro jezi namba 20.

Dakika ya 88,

Mamelodi wanafanya mabadiliko anatoka Marcelo Allende jezi namba 11 anaingia Rivaldo Coetzee jezi namba 40, anaingia Mosa Lebusa jezi namba 5 anatoka Sphelele Mkhulise jezi namba 21.

Dakika 90.

zimeongezwa dakika 6.

Dakika 90+3

Petro Atletico 0-2 Mamelodi Sundowns.

DAKIKA 90 ZIMEMALIZIKA

PETRO ATLETICO DE LUANDA 0-2 MAMELODI SUNDOWNS.

Popular Posts

Exit mobile version