NBC Premier League

LIVE: YOUNG AFRICANS vs AZAM FC

Mchezo wa Ligi kuu kati ya Young Africans dhidi ya Azam unaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Published on

Kick Off: 00″ Young Africans 0-0 Azam FC.

Dakika ya 01,

Azam wanakosa goli mpira uliookolewa na Dickson Job. Azam wanashindwa kutumia kona.

Dakika ya 4

Max Nzengeli anakosa goli kwa mpira mkali uliopigwa kuelekea lango la Azam, Max akipokea pasi kutoka kwa Pacome.

Dakika ya 8,

Yanga inapata goli kupitia kwa Aziz Ki.

Yanga 1-0 Azam FC.

Dakika ya 18,

Gibril Sillah anaisawazishia Azam kwa shuti kali nje kidogo ya kisanduku cha 18 lililomshinda golikipa wa Yanga, Gjigui Diarra, Pasi nzuri kutoka kwa Lusajo Mwaikenda.

Yanga 1-1 Azam FC.

Dakika ya 26,

Timu zote mbili zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 29

Aziz Ki anapiga shuti kali kuelekea langoni mwa Azam lakini golikipa Idrissu anaudaka mpira vyema.

Dakika ya 32

Feisal Salum anamfanyia madhambi Ibrahim Abbdullah Bacca.

Dakika ya 34:

Idris Abbdullah anapangua shuti kali la Aziz Ki aliyekunjuka vyema baada ya kupokea pasi kutoka kwa Pacome.

Dakika ya 36

Mudathir Yahya anakosa goli akiwa yeye na Golikipa wa Azam fc Idris Abdullah mpira unatoka nje.

Dakika ya 42.

Azam FC wanautawala mpira hadi hivi sasa.

Dakika ya

Feisal Salum anafanyiwa madhambi na kiungo wa Yanga Khalid Aucho nje kidogo ya eneo la 18.

Dakika ya 44,

Sidibe anapiga mpira wa moja kwa moja langoni mwa Yanga na kipa wa Yanga Djigui Diarra anaokoa inakuwa kona.

Dakika ya 45,

Sidibe anapiga mpira wa kona moja kwa moja nje, Dakika mbili (2) zimeongezwa.

MAPIMZIKO

YANGA 1-1 AZAM

KICK OFF: SECOND HALF

Dakika ya 45:

Yanga 1-1 Azam fc

Dakika ya 48

Yanga wanapata kona baada ya Malicku Ndoye kuokoa mpira wa Pacome uliokuwa unalenga lango la Azam fc.

Dakika ya 50,

Azam wanautawala mchezo.

Dakika ya 56,

Khalid Aucho anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Feisal Salum katikati ya uwanja,

Dakika ya 57,

Sospeter Bajana anapatiwa kadi ya njano.

Dakika ya 60

Azam wanapata Penalty baada ya Gibril Silla kufanyiwa madhambi na captain wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto anapewa kadi ya njano.

Dakika ya 62,

Goooal, Azam wanapata goli kupitia kwa Prince Dube kwa mkwaju wa Penalty.

Dakika ya 63

Feisal Salum anafanyiwa madhambi karibu na eneo la 18 na Mudathir Yahya, anapata kadi ya njano. Sidibe anapiga inaokolewa na Bakari mwamnyeto.

Dakika ya 64,

Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Mudathir Yahya anaingia Jesus Moloko.

Dakika 65,

Idrisu Abdullah anaokoa shuti kali la Maxi Nzengeli.

Dakika ya 66,

Aziz Ki anapiga mpira unaenda nje ya lango.

Dakika ya 67,

Lusajo anapewa kadi kwa kumfanyia madhambi Aziz Ki nje ya eneo la 18.

Dakika ya 68,

Aziz Ki anafunga goli kwa faulo kali nje ya 18, amemwacha golikipa wa Azam Idrisu Abdullah anagalagala tu, mpira ulikuwa na nguvu sana.

Dakika ya 71

Goaaaaaaaal, Aziz Ki anaipatia goli timu ya Yanga kwa mpira wa kuchop akipokea pasi safi toka kwa Khalid Aucho. Anapiga Hattrick hii leo.

Dakika ya 79,

Yanga 3-2 Azam fc

Dakika ya 83,

Yanga wanafanya mabadiliko, Anatoka Clement Mzize anaingia Zawad Mauya.

Dakika ya 87,

Azam wanafanya mabadiliko,

Anatoka : Sospeter Bajana.

Anatoka: Prince Dube

Anaingia: Iddi Nado

Anaingia : Idris Ilunga Mbombo

Dakika ya 89,

Yanga wanafanya mabadiliko,

Anatoka: Aziz Ki

Anaingia: Hafidhi Konkon

Dakika ya 90,

Zimeongezwa dakika 4

Yanga 3-2 Azam fc

Dakika ya 90+2

Diarra yupo chini anafanyiwa matibabu.

Dakika ya 90+4

Diarra bado yupo chini.

Dakika ya 90+5

Mpira unaendelea.

Dakika ya 90+^

Diarra anaokoa shuti kali la Bangala Yannick.

Dakika ya 90+7

Azam fc wanakosa goli kupitia kwa Yannick Bangala.

MPIRA UMEMALIZIKA>

YANGA 3-2 AZAM FC.

Popular Posts

Exit mobile version