Betting Tips

MKEKA POINT

Published on

Tottenham wametoka kushinda mchezo wao wa mwisho wa ligi na ni moja ya miche minne walioshinda kati ya 5 walizocheza hivi karibuni, hawajafungwa ila wana sare 1 tu. Ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Luton umewaweka hadi nafasi ya 4 ya msimamo wa EPL na wanajua ushindi leo utawasogeza hadi nafasi ya 3 juu ya Liverpool.

Fulham nao hawako mbali kimatokeo hivi karibuni, wakitoka kuwanyuka Sheffield United 3-1 pale Craven cottage. Kwenye michezo yao 5 ya mwisho, Wameshinda 3, wakipoteza mmoja na kutoa sare mmoja huku wakifunga mabao 6 na kuruhusu 4 tu kwenye michezo yao hiyo.

Spurs wamefunga mabao 12 na kuruhusu 6, lakini fomu yao waliyonayo sasa hivi inakupa jeuri ya kummfuata mazima mbele ya Fulham leo. Kati yao kuna GG za kutosha tu, Spurs akiruhusu nyavu zake kuguswa kwenye michezo 4 kati ya 5 na Fulham akiruhusu mabao 3.

TIP : SPURS WIN, OVER 2.5 NA BTTS(BOTH TEAMS TO SCORE)

Wakiwa nafasi ya 4 nyuma ya Juventus(3), Fiorentina wanajua ushindi wa zaidi ya magoli mawili utawasogeza hadi nafasi ya 3 na kummshusha Juventus, na ni jambo linalowezekana kwani wanacheza na miongoni mwa vibonde wa ligi, Empoli. Wakiwa na wastani mzuri wa kufunga(Magoli 11 kwa mechi 5), magoli zaidi ya 2 uhakika leo.

Kwenye michezo 5 ya mwisho, Empoli kashinda mchezo mmoja pekee, akifunga goli 1 tu huku akiwa karuhusu mabao 11. Kafungwa mechi 3 kati ya 5 na kutoa sare 1. Hakuna mechi yoyote aliyotoa BTTS hivyo halitarajiwi hilo leo mbele ya timu ambayo inafahamu mtaji wa magoli ya kufunga na kufungwa ni muhimu sana leo.

TIP : FIORENTINA WIN, OVER 2.5

Wote Valencia na Cadiz hawapitii nyakati bora sana kwenye msimu huu hadi nyakati hizi. Valencia akiwa na ushindi mmoja tu huku Cadiz akiwa hajashinda mchezo wowote kwenye michezo 5 iliyopita.

Lakini Valencia ana nafuu zaidi, hasa kwenye upatikanaji wa magoli, wamefunga magoli  6 na wao kuruhusu 7 huku Cadiz akiruhusu 8 na kufunga 3 pekee. Kwa asilimia hawa watu wanaweza wasifungane magoli mengi lakini pia siioni GG. Ila Valencia ana asilimia kubwa ya kushinda mchezo huu.

TIP : VALENCIA WIN, UNDER 2.5, NO GG(BTTS)

Popular Posts

Exit mobile version