Ofisa mtendaji mkuu wa klabu ya Real Madrid, Jose Angel Sanchez, amethibitisha kuwa hakuna uwezekano wowote kwa mshindi mara tano wa Ligi ya mabingwa Barani Ulaya Luca Modric kuondoka klabuni hapo licha ya kuhusishwa kujiunga na klabu mbalimbali kutoka Saudi Arabia na Inter Miami ya Marekani mwezi January.
Hakuna mazungumzo yoyote tuliyofanya na klabu kutoka Saudia yanayomuhusisha Luca Modric kuondoka mwezi january, na hatujui kama ataondoka lini kwenye kikosi chetu.
CEO wa Real Madrid akizungumza kuhusu Modric.
Wakati Real Madrid ikilitolea ufafanuzi swala la nyota huyo kutokuondoka mwezi January, Mkongwe Modric yeye ameweka wazi kuwa hafurahishwi na muda wa kucheza anaopata chini ya Carlo Ancellot msimu huu. Hii inamaanisha kuwa huenda nyota huyo akachukua maamuzi ya kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Luca Modric atakuwa sehemu ya kikosi cha Real Madrid kitakacho ikabili SC Braga kwenye usiku wa Ulaya Jumanne, October24.