AFL

KISA ENYIMBA CAF YAPANGUA RATIBA AFL

Published on

Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF imeamua leo Jumanne kuahirisha mechi kati ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco dhidi ya Enyimba ya nchini Nigeria ambayo ilikuwa kwa ajili ya kukamilisha hesabu ya matokeo ya jumla ya mchezo huo uliopangwa kuchezwa hapo kesho, katika uwanja wa Mohammed V

Hii inatokana na kuchelewa kuwasili kwa timu ya Enyimba nchini Morocco. Taarifa zinasema kuwa klabu hiyo kutoka nchini Nigeria imeshindwa kutua nchini Morocco kutokana na kukosa kibali cha kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Murtala Mohammed

Kwa sasas timu imerejea hotelini ikiwa imetumia saa 6 na dakika 30 kwenye ndege ya Chattered ikisubiri kibali cha kutua kutoka kwa Mamlaka za Morocco ili iweze kuondoka bila mafanikio. Ikumbukwe katika mchezo wa awali klabu ya Enyimba ikiwa nyumbani ilikubali kichapo cha 0-1.

Sasa mchezo huo utachezwa siku ya Alhamis siku ya tarehe 26 oktoba katika uwanja wa Mohammed V, sambamba na mchezo kati ya Esperance Sportive de Tunis na TP Mazembe ambao mchezo wa awali ulichezwa jijini Dar Es Salaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo TP Mazembe waliutumia kama uwanja wao wa nyumbani na kupata ushindi wa bao 1-0

Popular Posts

Exit mobile version