Ligi ya mabingwa Barani Ulaya inatarajiwa kurindima hii leo kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja tofauti tofauti.
19:45 INTER MILAN vs RB SALZBURG
Inter Milan hadi hivi sasa chini ya Simone Inzaghi haijapoteza mchezo wowote katika michezo miwili (2) ya kundi D, ipo nafasi ya pili ya msimamo wa kundi hilo ikiwa na alama nne (4) ikiwa na alama sawa na kinara wa kundi hilo Real Sociedad.
RB Salzburg hadi hivi sasa chini ya kocha Gerhard Struber haijapata ushindi katika michezo yake mitatu ya mwisho ya kimashindano, wametoka sare mara moja (1) na kupoteza mara mbili ikiwemo kipigo kitoka kwa Real Sociedad cha goli 2-0, katika michezo ya kundi D wameshinda mchezo mmoja pekee na ipo katika nafasi ya tatu (3) ya msimamo.
Hii itakuwa mara ya tatu (3) kwa timu hizi kukutana,
- Inter Milan imeshinda michezo miwili iliyopita
- Salzburg hawajapata ushindi katika michezo yake mitatu ya mwisho ya kimashindano, wakipoteza mara mbili (2) na kupata sare moja (1).
- Inter Milan haijapoteza michezo 11 kati ya 12 iliyopita ya kimashindano wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani tangu mwezi April, wakipata ushindi mara tisa (9) na sare mbili.
- Salzburg hawajapoteza mchezo wowote wakiwa ugenini kwenye mashindano yote msimu huu, wakishinda mara saba (7), na sare mbili (2) katika michezo yake nane iliyopita.
22:00 SEVILLA vs ARSENAL (Group B)
Sevilla itakua mwenyeji wa Arsenal hii leo kwenye mchezo wa kundi B katika dimba la Ramon Sanchez Padjuan nchini Hispania. Timu hizi zimekutana mara mbili (2) katika michuano hii na kila timu ikishinda mara moja (1).
- Arsenal imeifunga Sevilla magoli manne (4) katika michezo miwili waliyokutana.
- Sevilla imeifunga Arsenal magoli matatu (3) katika michezo miwili waliyokutana.
- Mara ya mwisho kukutana kwenye michuano ya UEFA timu hizi zilikuwa zimepangwa kundi H na matokeo yalikuwa Sevilla 3-1 Arsenal huku mchezo wa kwanza Arsenal ikishinda 3-0 Sevilla.
- Arsena haijapata ushindi wowote ikiwa ugenini katika mashindano haya tangu mwaka 2016 walipoifunga FC Basel.
- Je, leo ataendeleza unyonge wake akiwa ugenini ?.
19:45 GALATASARAY vs BAYERN MUNICH (Group B)
- Galatasaray wanaingia katika mchezo huu wakiwa hawana rekodi ya kupoteza mchezo wowote msimu huu.
- Galatasaray hii leo wanaingia wakiwa na maorali ya kutosha baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wa Dabi dhidi ya Besiktas.
- Bayern Munich tangu ipokee kipigo cha goli 3-0 kwenye mchezo wa Supercup dhidi ya RB Leipzing mwezi Agosti, haijapoteza mchezo wowote.
- Bayern wanaifuata Galatasaray wakiwa na nguvu kubwa kwenye eneo la ushambuliaji, Harry Kane hadi hivi sasa amefunga magoli 10 katika mashindano yote msimu huu amefunga magoli tisa (9) katika michezo nane (8) ya Ligi kuu nchini Ujerumani.
22:00 MANCHESTER UNITED vs FC COPENHAGEN (Group B)
- Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa msimu wa 2006/07 kwenye michuano ya Ulaya, Manchester United akishinda nyumbani 3-0 na kupoteza ugenini 1-0.
22:00 UNION BERLIN vs NAPOLI
22:00 BRAGA vs REAL MADRID
22:00 RC LENS vs PSV EINDHOVEN
22:00 BENIFICA vs REAL SOCIEDAD.