Jude Bellingham ni mchezaji wa pili kufunga bao katika mechi zake tatu za kwanza za Ligi ya Mabingwa barani Ulaya akiwa na Real Madrid. Bellingham alifunga goli lililokuwa la ushindi wakati kikosi cha Madrid kikipata ushindi muhimu wa magoli 2-1 ugenini dhidi ya Braga.
Kwa sasa Jude Bellingham amefikisha jumla ya magoli 11 na pasi za usaidizi wa magoli 3 katika michezo yake 12 ya kwanza kwa klabu yake ya Real Madrid. Magoli katika mechi tatu zilizofuatana dhidi ya Union Berlin, Napoli na Braga, yalitosha kabisa kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufikia rekodi hiyo tangu Christian Karembeu mwaka wa 1998.
Ni miaka 25 sasa tangu mara ya mwisho mchezaji wa Real Madrid kuweka rekodi hii hadi alipofanya hivyo Jude Bellingham hapo jana dhidi ya Braga.