Betting Tips

MKEKA POINT

Published on

Barcelona wameshinda 1-0 kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Bilbao lakini pia walishinda 1-0 kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi ya mabingwa dhidi ya Porto. Mfululizo huu unakuonyesha Barcelona hawafungi magoli mengi, wamefunga magoli  7 tu kwenye michezo 5 ya mwisho.

Hadithi ni tofauti kwa Shakhtar Donetsk, wanetu kabisa hawa, wameshinda 3-0 kwenye mchezo wao mwisho wa ligi lakini itakumbukwa waliwafunga Royal Antwerp 3-2 kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa wa mwisho kabla ya leo. Wanafunga na kufungika pia.

TIP: NENDA NA MAGOLI ZAIDI YA  2.5 AU WAFUNGANE(BOTH TEAMS TO SCORE)

PSG walipigwa vibaya sana na Newcastle kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi ya Mabingwa Dhidi ya Newcastle, lakini ushindi wa 3-0 dhidi ya Strasbourg  pengine utawarudisha kwenye ari dhidi ya AC Milan leo. Licha ya matokeo ya ushindi kwenye mechi 3 kwenye michezo mitano(5) ya mwisho, lakini haikupi uhakika wa PSG kushinda leo kutokana na kusuasua kwao. Hapa sikushauri sana.

Wapinzani wa AC Milan wametoka kupoteza mchezo wao wa  Serie A dhidi ya Juventus na itakumbukwa sare ya 0-0 dhidi ya Dortmund kwenye ligi ya mabingwa. Wamefunga magoli 6 tu na kuruhusu 2 kwenye michezo yao mitano(5) ya mwisho. Wavivu kufunga na wagumu kufungika magoli mengi pia. Magoli pia sio ya kuyabetia sana kwenye mechi hii.

TIP : MAGOLI CHINI YA  2.5 AU WAFUNGANE(BOTH TEAMS TO SCORE)

Wako nyumbani leo Magpies tena, wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kusambaratisha PSG 4-1, wanakutana na Dortmund waliotoka 0-0 dhidi ya AC Milan. Wote wanaitaka hii mechi. Newcastle kashinda mechi 4 kati ya 5 na hajafungwa hata 1 ni kama walivyo wapinzani wao tu. Kimeumana leo.

Newcastle kafunga magoli 13 na kuruhusu matatu tu. Dortmund karuhusu matatu tu pia na akifunga mabao 9 kwenye michezo 5 iliyopita. Wote wanaitaka mechi, wote wanafunga.

TIP : NEWCASTLE USHINDI NA MAGOLI ZAIDI YA 2.5

Popular Posts

Exit mobile version