African Football League

AFL KUENDELEA HII LEO AFRIKA.

TP Mazembe itashuka dimbani hii leo kuitafuta tiketi ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya AFL dhidi ya Esperance de Tunis.

Published on

Leo michezo miwili ya African Football League hatua ya Robo fainali inatarajiwa kuendelea kwa michezo miwili kuchezwa katika viwanja viwili tofauti Barani Afrika. Esperance watakuwa wenyeji wa Enyimba hii leo na Esperance watakuwa wenyeji wa TP Mazembe.

Hizi ni takwimu za michezo miwili ya leo ya AFRICAN FOOTBALL LEAGUE.

18:00 ESPERANCE vs TP MAZEMBE

  • Timu hizi zimekutana mara tisa (9) katika michuano ya kimataifa
  • Kila timu imeshinda mara tatu na zimetoa sare mara tatu.
  • TP Mazembe imeifunga magoli mengi zaidi katika mchezo mmoja dhidi ya Esperance mchezo ambao ulimalizika kwa 5-0.
  • Katika michezo mitano (5) ya mwisho ambayo TP Mazembe imecheza, imeshinda michezo mitatu (3), na imepoteza michezo miwili (2).
  • Esperance imeshinda michezo mitatu (3), imetoa sare mechi moja (1), na imepoteza mchezo mmoja (1).
  • Mara ya Mwisho timu hizi kukutana ilikuwa katika dimba la Benjamin Mkapa, TP Mazembe ilishinda goli 1-0 katika mashindano haya.
  • Mshindi wa Jumla ataenda kukutana na mshindi wa mchezo wa Enyimba na Wydad Casablanca.

21:00 WYDAD CASABLANCA vs ENYIMBA

  • Timu hizi mbili zimekutana mara moja katika michuano ya kimataifa.
  • Wydad Casablanca imeshinda mchezo mmoja, Enyimba haijawahi kupata ushindi mbele ya Wydad AC.
  • Katika michezo mitano (5) ya mwisho ambayo Wydad AC imecheza kwenye mashindano yote, imeshinda michezo minne (4), imetoa sare mchezo mmoja (1).
  • Enyimba imeshinda mchezo mmoja (1), imepoteza michezo mitatu (3), imetoa sare mchezo mmoja (1), katika michezo mitano (5) ya mwisho.
  • Mara ya mwisho timu hizi kukutana Enyimba ilikuwa nyumbani na ilikubali kichapo cha goli 1-0.
  • Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa mchezo wa Esperance dhidi ya TP Mazembe.

Popular Posts

Exit mobile version