Yanga

NANI MCHEZAJI BORA WA MWEZI YANGA ?.

Nyota wa klabu ya Yanga, Aziz Ki Stephane, Maxi Nzengeli na Dickson Job wametajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwa mwezi October.

Published on

Klabu ya Yanga kupitia kwa Ofisa habari na mawasiliano wake Ally Shaban Kamwe imetangaza majina matatu ya nyota wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi October, majina ya wachezaji hao ni Stephane Aziz Ki, Dickson Job na Max Nzengeli.

Yanga imecheza michezo minne (4) kwa mwezi October, imepata ushindi katika michezo mitatu (3) na imepoteza mchezo mmoja. Tuzo hiyo inapigiwa kura na mashabiki wa klabu kupitia Application wa Yanga.

Wachezaji waliotajwa kuwania tuzo hiyo wawili wanacheza katika eneo la ushambuliaji na mmoja anacheza katika eneo la ulinzi.

DICKSON JOB

  • Anacheza eneo la kati la Ulinzi
  • Akiwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Yanga, Timu yake haijapoteza mchezo wowote mwezi October, ameiongoza Yanga kushinda katika michezo yote mitatu (3) aliyoitumikia, mchezo dhidi ya Ihefu ambao timu yake ilipoteza alikuwa benchi.
  • Michezo yote mitatu aliyoanza Dickson Job, Yanga imefungwa magoli mawili (2) pekee.

MAX NZENGELI

  • Anacheza eneo la ushambuliaji, mara nyingi akicheza eneo la kiungo akitokea pembeni mwa uwanja.
  • Ameitumikia Yanga katika michezo mitatu (3) mwezi huu, na katika michezo yote aliyoanza timu yake imeshinda, katika mchezo iliyopoteza mbele ya Ihefu alianzia benchi.
  • Yanga imefunga magoli nane (8) katika michezo hiyo mitatu (3) ambayo Max ameanza, akitoa pasi za usaidizi moja (1) na amefunga magoli mawili (2).

STEPHEN AZIZ KI

  • Anacheza eneo la ushambuliaji, mara nyingi anacheza karibu na mshambuliaji wa mwisho.
  • Ameanza katika michezo mitatu (3) ya timu hiyo kwa mwezi huu na timu hiyo imeshinda michezo yote, wakati Yanga inapoteza mbele ya Ihefu mapema mwanzoni mwa mwezi alianzia benchi.
  • Yanga imefunga magoli nane (8) katika michezo hiyo mitatu (3) ambayo Aziz Ki ameanza, hajatoa pasi ya usaidizi wa goli na amefunga magoli manne (4).

Yanga imeingia makubaliano na shirika la nyumba la NIC mapema mwezi huu kwaajili ya kutoa tuzo za mwezi kwa mchezaji aliyefanya vizuri zaidi ndani ya klabu hiyo.

Popular Posts

Exit mobile version