NBC Premier League

SIMBA USO KWA USO NA IHEFU LEO.

Klabu ya Simba haijawahi kupoteza katika mchezo wake dhidi ya Ihefu, leo watashuka tena dimbani saa moja Jioni.

Published on

Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inataraji kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja kuchezwa katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar Es Salaam. Hizi ni takwimu za timu zote mbili kuelekea katika mchezo huu mkubwa.

19:00 SIMBA vs IHEFU

UWANJA: Benjamin Mkapa

  • Timu hizi mbili zimekutana mara tano (5), katika michezo yote hiyo klabu ya Simba imeshinda michezo yote mitano (5) na Ihefu haijawahi kupata ushindi ama sare yoyote ile mbele ya Simba.
  • Ihefu hadi hivi sasa imecheza michezo sita (6) ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara, imeshinda michezo miwili ikiwemo mmoja dhidi ya Young Africans waliposhinda 2-1 wakiwa nyumbani Mbarali, imetoka sare mchezo mmoja (1) na imepoteza michezo mitatu (3), ipo nafasi ya 11 ya msimamo wa Ligi ikiwa na alama saba (7).
  • Ihefu imefunga magoli matatu (3) na kufungwa magoli matano (5) hadi hivi sasa.
  • Ihefu inaingia katika mchezo huu ikiwa imetoka kumfuta kazi kocha wake mkuu Zuberi Katwila na sasa itakuwa chini ya Kocha kutoka Uganda Moses Basena.
  • Simba ipo nafasi ya pili (2) ya msimamo wa Ligi ikiwa na alama 15 nyuma ya kinara Young Africans.
  • Simba imecheza michezo mitano (5), ikiwa ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hadi hivi sasa wa kutoa sare kwenye Ligi kuu.
  • Simba imefunga magoli 14 na kuruhusu magoli manne (4) chini ya kocha Robert Oliviera.
  • Simba imeifunga Ihefu magoli nane (8), na imefungwa goli moja (1).
  • Mchezo wa mwisho kuzikutanisha timu hizi ilikuwa katika Mbarali, Jijini Mbeya wakati Simba ikishinda goli 2-0.
  • Ushindi mkubwa ambao Simba iliwahi kupata dhidi ya Ihefu ulikuwa ni wa goli 5-1, kwenye michuano ya FA katika Dimba la Mkapa (April 7, 2023).

Popular Posts

Exit mobile version