Usiku wa kuamkia leo Bingwa wa dunia wa uzito wa juu wa [WBC ]Tyson Fury alimshinda bondia wa zamani wa [UFC ] Francis Ngannou kwa uamuzi wa Majaji wawili kwa mmoja katika pambano lisilo la ubingwa lililochezwa nchini Saudi Arabia ,pambano ambalo watu wengi waliamini Ngannou alistahili ushindi.
Ngannou alimwangusha Tyson katika raundi ya tatu kwa [ left hook ] ingawa haikuamua mwenendo wa pambano kwa asalimia kubwa lakini ni kama pambano lote lilitawaliwa na Ngannou kwa ambao wameangalia pambano hilo hata ukiuliza zaidi ya mara tatu bado Ngannou alistahili kushinda .
Baada ya pambano kumalizika uamuzi wa Majaji ulikuwa hivi
Jaji wa kwanza alitoa [95-94 ] kwa Ngannou ,
Majaji wengine walitoa [96-93] na [95-94 ] kwa Fury
Maoni ya wadau wakubwa wa mchezo wa ngumi wanaamini kwamba mechi hiyo ilipangwa kwa ajili ya Fury kushinda kwa sababu ni bondia wa Uingereza lakini alizidiwa kwa kila kitu.
Baada ya pambano kumalizika Fury amesema hakuna kipengele cha mchezo wa marudiano lakini anatamani kupigana tena na Ngannou
Bondia Tyson Fury ana pambano la ubingwa wa uzito wa juu dhidi ya Oleksandr Usyk mjini Riyadh katika tarehe ambayo bado haijatangazwa rasmi lakini huenda ikawa Desemba 23.