Makala Nyingine

MKAPA KUTUMIKA KIMATAIFA TU, MASHABIKI WATOA MAONI

Published on

Mashabiki wa soka nchini wamejikuta kwenye sintofahamu baada ya kauli kutoka kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Damas Ndumbaro juu ya matumizi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Taarifa ikisema kuwa Uwanja huo utatumika kwa kwa ajili ya michezo ya Timu za Taifa na Mechi za Kimataifa za Vilabu za CAF na si vinginevyo na mchezo wa Watani wa Jadi kati ya Simba na Yanga wa tarehe 5/11/2023, ndio utakuwa mchezo wa mwisho wa ligi kuu kupigwa kwenye Dimba hilo kwa mujibu wa taarifa.

Lengo kuu ni kuhakikisha uwanja wetu unabaki kuwa kwenye kiwango bora cha kuweza kuwa mwenyeji wa michezo mingi ya hadhi ya kimataifa. Tunaelekea kwenye kuukarabati uwanja ufikie matakwa ya CAF na FIFA na ndio maana tunaupunguzia matumizi na ubaki kutumika kwenye michezo maalumu ya Kimataifa.

Alisema Waziri Ndumbaro

Mpango huu ulipokelewa kwa mitizamo tofauti na baadhi ya wadau wa soka

Nadhani sio wazo baya kutoka kwa serikali kwa kuwa nia ni kuwa na uwanja bora wa kisasa. Si umeona mwenyewe watu kama TP Mazembe wanakuja kuomba kuutumia uwanja wetu, akina Al Hilal ni kwasababu uwanja wetu unapendeza saivi. Ni wakati sasa vilabu vyetu hivi Simba na Yanga nao watafute viwanja vyao sasa. Hili ni kama changamoto kwao.

Shabiki mwingine alisema kuwa pamoja na kuwa ni wazo zuri lakini kama limekuja kwa kushtukiza  na watakosa kuona burudani kwenye dimba hilo.

Tushazoea kuziangalia timu zetu kwenye dimba la Mkapa zikicheza vizuri na kutakata kuliko kwenye viwanja vingine, tutamissi hiyo burudani ni kama imekuja ghafla. Mwanzoni nilivyosikia nikahisi hadi mechi ya keshokutwa (5/11/2023), pia haitochezwa hapo. Lakini kwakuwa serikali ndiyo wenye uwanja wao na wameamua hivyo basi hatuna namna.

Walimaliza kusema mashabiki hao.

Popular Posts

Exit mobile version