Promota wa Tyson Fury, Frank Warren mapema baada ya pambano la bondia wake na Francis Ngannou alitoa taarifa kuwa huenda pambano la Tyson Fury na Oleksandr Usyk lililokuwa limepangwa kufanyika December 23 katika mji wa Riyadh nchini Saudi Arabia likaahirishwa baada ya Fury kushinda kwenye pambano zito dhidi ya Francis Ngannou.
Tunaenda kupigana na Usyk December 23, nina mashaka huenda pambano lisiwepo, Tyson hawezi kwenda Camp baada ya pambano zito kama lilie, ni wiki nane (8) tu zimesalia. Anahitaji muda wa kuuweka mwili wake sawa arudi kwenye hali yake ya kawaida, ngoja tusubiri, lakini kurudi camp itakuwa ni mwakani.
Alisema Frank Warren, Promota wa Fury.
Tuna mkataba unaosema pambano litafanyika December 23. Ngoja aachie taji lake kwanza harafu ndio apumzike.
Bondia Oleksandr Usyk alisma.
Mapema leo promota wa Oleksandr Usyk ametoka hadharani na kusema kuwa pambano hilo litakuwepo kama lilivyokuwa limepangwa na hakuna namna Tyson Fury atalikwepa hili.
Pambano lipo pale pale December 23, hakuna namna ambayo Fury anaweza kulikwepa hili.
Promota wa Oleksandr Usky alisema.