Yanga

AZIZ KI MCHEZAJI BORA WA YANGA OKTOBA.

Nyota wa klabu ya Yanga Stephane Aziz Ki ametangazwa kuwa mchezaji bora wa klabu ya Yanga kwa mwezi Oktoba.

Published on

Klabu ya Yanga imemtangaza nyota wake Stephane Aziz Ki kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba akiwashinda Dickson Job na Max Nzengeli kwenye kinyang’anyiro hicho. Hizi ni tuzo za kwanza kutolewa na klabu hiyo kupitia kwa mdhamini wa tuzo hizo shirika la nyumba la Taifa (NHC). Tuzo hizo zimetolewa kwa kuzingatia kura za mashabiki ambazo zilipigwa katika application ya klabu hiyo.

Aziz Ki amebeba tuzo hiyo baada ya kucheza michezo mitatu (3) ya timu hiyo kwa mwezi huu na timu hiyo imeshinda michezo yote. Yanga imefunga magoli nane (8) katika michezo hiyo mitatu (3) ambayo Aziz Ki ameanza, hajatoa pasi ya usaidizi wa goli na amefunga magoli manne (4).

Aziz Ki atashuka dimbani na kikosi cha Yanga Jumapili hii ya November 5 katika mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya mtani wake klabu ya Simba katika dimba la Benjamin Mkapa. Yanga kwasasa inaongoza kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 18 huku Simba ikiwa nafasi ya pili na alama 18 lakini ikiwa pungufu ya mchezo mmoja.

Popular Posts

Exit mobile version