Top Story

JKT QUEENS KUONDOKA KESHO ALFAJIRI.

Klabu ya JKT Queens kuianza safari kesho Alfajiri kuelekea nchini Ivory Coast kwaajili ya michuano ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika kwa upande wa wanawake.

Published on

Klabu mwakilishi wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, JKT Queens itaondoka kesho Alfajiri kuelekea nchini Ivory Coast kwaajili ya michuano ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika. Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Afisa habari wa klabu hiyo Massau Bwire amesema nyota wanaotumika kwenye kikosi cha timu ya Taifa huko nchini Botswana baada ya mechi ya leo wataunganisha hadi nchi Ivory Coast.

Timu yetu ya JKT Queens saa 10:00 Alfajiri kesho, itaondoka hapa nchini kuelekea Ivory coast kwa ndege ya Ethiopia Airline, ambapo wataondoka moja kwa moja mpaka Ivory coast, kama mnavyofahamu timu yetu ya taifa, Twiga stars leo itakuwa na mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya taifa ya Botswana katika mji wa Gaborone … Tunao wachezaji wetu 16 huko, wao wataondokea kule kwenda Ivory coast, wao wataondoka tarehe 1, saa 9:30 mchana kuelekea Abdjan.

Afisa Habari wa JKT Queens, Massau Bwire akizungumzia safari ya JKT Queens kuelekea Ivory Coast.

JKT Queens ni miongoni mwa timu nane zitakazoshiriki mashindano haya ya Ligi ya mabingwa Baran Afrika, JKT ipo kundi A la michuano hiyo ikiwa na Sporting Club Casablanca (Morocco), Atletico Abdjan (Ivory Coast) na Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini).

JKT Queens itafungua dimba November 5 majira ya saa tano usiku 5:00 dhidi ya Mamelodi Sundowns ladies kutoka Afrika Kusini, na baadae itacheza November 8, saa 2:00 usiku dhidi ya Atletico Abidjan, na mchezo wa mwisho utawakutanisha na Sporting Club Casablanca November 11.

Lengo letu na dhamira yetu ni kuona vijana wetu wanacheza fainali November 19.

Afisa Habari wa JKT QUEENS, Massau Bwire.

Popular Posts

Exit mobile version