Top Story

KIEMBA: MESSI HAKUSTAHILI BALLON D’OR

Mkongwe Amri Kiemba amesema Messi hakustahili kubeba tuzo ya mchezaji bora msimu huu.

Published on

Kupitia kipindi cha Michezo cha Hili game kinachorushwa na Clouds fm mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Simba Amri Kiemba ametoa maoni yake baada ya zoezi la utoaji tuzo za mchezaji bora wa Dunia ( Ballon d’or) iliyofanyika Jijini Paris nchini Ufaransa na kusema Messi hakustahili kuingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo hiyo.

Messi hata kuingia humu sijui ameingiaje ,kwa michuano ya wiki tatu wiki nne ingekuwa inatumika, Ronaldo hadi sasa hivi hajawahi kuchukua World Cup na miaka mingine aliyochukua Ballon D’Or ni miaka ambayo World Cup imefanyika.

Hapo unaona kigezo sio World Cup, kigezo kilikuwa ni performance ya msimu na ukija kwenye hilo Messi humuoni akiingia ,kwa mafanikio aliyoyapata mwaka husika tuzo ni ya Haaland.

Amri Kiemba kuhusu tuzo ya Ballon d’Or kupatiwa Leonel Messi.

Popular Posts

Exit mobile version