Taifa Stars

TANZANIA KUWANIA TUZO YA TIMU BORA AFRIKA.

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imewekwa kwenye kipengele cha tuzo ya timu bora ya mwaka Barani Afrika, tuzo zinazotolewa na shirikisho la soka Afrika CAF.

Published on

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya timu ya Taifa bora Barani Afrika, kwa mwaka 2023 kwenye tuzo zinazotolewa na shirikisho la soka Barani Afrika. Tuzo hizo zitatolewa December 11 katika mji wa Marrakesh nchini Morocco.

Tanzania inawania tuzo hiyo sambamba na mataifa ya Cape Verde, Gambia, Guinea Bissau, Equatorial Guinea, Mauritania, Morocco, Msumbiji, Namibia na Senegal. Tanzania ndio nchi pekee kutoka Afrika Mashariki inayoshiriki katika kinyang’anyiro hicho.

Popular Posts

Exit mobile version