Top Story

YANGA, DIARRA WATAJWA TUZO ZA AFRIKA.

Klabu ya Yanga imeingia kwenye kipengele cha kuwania tuzo ya klabu bora ya mwaka 2023 na Mlinda lango wake Djigui Diarra katika kipengele cha mlinda lango bora.

Published on

Kuelekea usiku wa tuzo za shirikisho la soka Barani Afrika, nafasi mbalimbali zimetajwa kwenye makundi mbalimbali yanayowania tuzo hizo.

Klabu ya Yanga imetajwa kuwania kipengele cha timu bora ya mwaka ya klabu 2023, ikiwa sambamba na klabu za CR Belouzdad, USM Alger, Asec Mimosas, Al Ahly, Raja Casablanca, Wydad AC, Mamelodi Sundowns, Marumo Gallants, Esperance de Tunis na Yanga ya Tanzania.

Pia shirikisho la soka Barani Afrika limemtaja mlinda mlango wa Yanga na timu ya Taifa ya Mali Djigui Diarra kuwania tuzo ya golikipa bora wa mwaka 2023 Barani Afrika akiwa sambamba na Mohamed El Shenawy (Misri), Yassin Bounou (Morocco), Andre Onana (Cameroon), Ronwen Williams (Afrika Kusini), Eduard Mendy (Senegal), Oussama Benbot (Algeria), Youssef El Motie (Morocco), Pape Mamadou (Senegal), na Landing Badji (Senegal).

Fiston Kalala mayele aliyekuwa anaitumikia Yanga kabla ya kutimka klabuni hapo na kwenda Pyramids na Djigui Diarra wametajwa kuwania tuzo katika kipengele cha mchezaji bora wa mashindano ya klabu kwa mwaka 2023, tuzo hizi zinahusu michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika na kombe la shirikisho.

Popular Posts

Exit mobile version