Serikali ya nchini Colombia chini ya Rais Gustavo Petro, leo imetangaza kuwa kundi la ELN ndilo linalohusika kummshikilia mateka baba mzazi wa mchezaji wa Liverpool, Luis Diaz, Mzee Luis Manuel Diaz ambaye alitekwa sambamba na mkewe, Cilenis Marulanda(mama mzazi wa Luis Diaz) walipokuwa kwenye kituo cha mafuta kilichopo Barrancas.
Juzi wananchi kadhaa akiwemo baba mzazi wa Luis Manuel Diaz, ambaye ni babu wa Luis Diaz, Alfonso Diaz, waliandamana mtaani wakiwa wamevaa fulana zenye picha ya Luis Manuel Diaz kwa ajili ya kupaza sauti kuachiwa kwa mwenzao huyo wa hapo maeneo ya Barrancas huku wakionyesha pia kusononeshwa na tukio hilo.
Taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa serikali ipo kwenye mazungumzo ya amani ya kutafuta suluhu ili watekaji waweze kumuachia raia wao huyo ambaye ni baba mzazi wa Luis Diaz.