EPL

ANTHONY TAYLOR APIGWA CHINI EPL.

Published on

Mwamuzi Anthony Taylor ameshushwa kutoka kuchezesha mechi za Ligi Kuu nchini Uingereza hadi Ligi ya Championship baada ya kuwazawadia Newcastle penati yenye utata dhidi ya Wolves siku ya Jumamosi.

Kwa sasa mwamuzi huyo atasimamia pambano la daraja la pili kati ya Preston na Coventry wiki moja baada ya mgawanyiko huo. Taylor alikashifiwa baada ya kuwapa wageni penati katika uwanja wa Molineux, ambayo iliwafanya Magpies kuongoza katika kipindi cha kwanza.

Mwamuzi huyo alipuliza kipyenga na kulekeza eneo la penati baada ya Hwang Hee-chan kumwangusha Fabian Schar alipokuwa akijaribu kuondoa mpira, na uamuzi wake ukapingwa na VAR. Afisa wa zamu Stockley Park Jarred Gillett alichukua muda wake lakini hatimaye akachagua kutomuamini Taylor na akaamua kumtuma mtu wake kutazama tukio hilo kwa mara ya pili.

Wolves hawakuweza kunyakua ushindi huku wakimaliza kwa sare ya 2-2 wakiwa nyumbani, lakini walitoka nyuma mara mbili na kuhakikisha hawapotezi pointi tatu. Gary O’Neil ambaye hapo awali amekuwa muwazi kuhusu masuala ya waamuzi baada ya Wolves kupokea maamuzi mawili yenye utata dhidi ya Manchester United na Luton Town msimu huu.

Bao la pili (la Newcastle) halikuwa penalti kamwe, Ulikuwa uamuzi mbaya uwanjani na kutoka kwa VAR lakini tulifanikiwa kurejea mchezoni.

Gary O’Neil aliiambia Sky Sports

Nilijaribu kuondoa mpira na nikaona mtu akinizuia. Nilisimama na akanigusa – sidhani kama ilikuwa penati. Nilijisikia huzuni na nilitaka sana kufanya kitu kwa ajili ya timu yangu. Kila mtu alisema ‘Unaweza kufanya hivyo na bado ukawa bora uwanjani. Walinipa imani na nikafunga.

Hwang – ambaye alifunga bao la kusawazisha – alisema kuwa ‘amehuzunishwa’ na uamuzi huo.

Kucheleweshwa kwa maamuzi kwa muda mrefu, inamaana kuwa ilikuwa ngumu kwa mwamuzi kufanya maamuzi.

Kocha wa Newcastle Eddie Howe alikiri.

Taylor sio afisa wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu kushushwa kwenye michuano hiyo kutokana na uzembe na maamuzi tata. Adrian Holmes alisimamia mechi ya nyumbani ya Millwall dhidi ya Hull mnamo Oktoba, baada ya kudhani kimakosa bao la Luis Diaz lilikuwa ni la kuotea wakati Liverpool ilipokutana na Tottenham kaskazini mwa jiji la London.

Popular Posts

Exit mobile version