Dodoma Jiji wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-1 dihidi ya KMC kwenye dabi ya “Halmashauri za Manispaa” na kuwafanya Dodoma Jiji kufikisha alama 15 na kuwashusha KMC kwenye nafasi ya 4 ya msimamo wa ligi kuu ya NBC kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Uhuru.
KMC waliatanguliwa mapema tu kwa goli zuri la Zidane Sereri dakika ya 3, akiunganisha kwa bega mpira ulionekana kafunga kwa kichwa, lakini haikujalisha.
Dodoma Jiji wakionyesha kiu ya kupata matokeo, hawakupoa na kufanya mashambulizi mfululizo. Kutoka kwenye mpira wa adhabu walioupata KMC wakashindwa kuutumia, shambulizi la kushitukiza likiongozwa na Mwana Kibuta David, akipiga pasi murua na kummkuta mfungaji Emmanuel Martin akitokea upande wa kushoto na kupiga shuti kali la chinichini lililommshinda golikipa Denis Richard. 2-0 Dodoma Jiji.
KMC walionekana kukosa utulivu kabisa kwani hata nafasi chache walizokuwa wakijaribu kuzitengeneza hawakuweza kuzitumia na nyingi kuwa faida kwa Dodoma Jiji.
Dakika ya 31, KMC walifanikiwa kurejesha goli 1, kona iliyochongwa vizuri na Nahodha Awesu Awesu ilimmkuta Rashid Chambo, aliyeukwamisha mpira kimiani kwa kichwa akiwaacha golikipa Aaron Kalambo na walinzi wake wakilaumian. KMC 1-2 Dodoma Jiji
Rashid Chambo aliachia mkwaju dakika ya 42 lakini golikipa Kalambo alikuwa imara. Safari hii kona haikuzaa matunda.
Mapumziko KMC 1-2 Dodoma Jiji
KMC walirudi kipindi cha pili kwa kasi ya kutaka kusawazisha mapema lakini Dodoma Jiji walikuwa imara. Mwalimu Moalin aliwaingiza Redemtus Mussa, Tepsi Evance na Waziri Junior kwaajili ya kuongeza presha ya mashambulizi, hata hivyo Joram Mgeveke na safu yake ya ulinzi walikuwa makini.
Dodoma Jiji walikuwa na kazi kubwa ya kuzuia mashambulizi ya KMC ambao walionekana kucharuka kipindi hiki cha pili. Wakafanya mabadiliko kwenye safu ya ushambuliaji ili kuzidisha presha kwenye ushambuliaji na kuwaqpunguza kazi KMC kushambulia wakimuingiza Paul Peter.
Mpira ukionekana kuchezwa zaidi kwenye eneo la pembeni baada ya kuwa na viungo wengi sana katikati ya uwanja, ililazimu kufanyika hivyo ili kuufungua uwanja. Walimu wote walikuwa na mbinu za kufanana muda huu, wakiweka washambuliaji kuzuia kasi za wapinzani kuanzia juu lakini kuhakikisha pia katikati ya uwanja wote wanakuwa wagumu kupitika.
Dodoma Jiji wakafanikiwa kujipambania na kuhakikisha wanaondoka na ushindi. Mpaka dakika 90 za mchezo zinatamatika, KMC wakakubali kichapo cha 2-1 kutoka kwa Dodoma Jiji. Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Dodoma Jiji wakiwa ugenini.
Kwingineko kwenye dimba la Manungu, Morogoro, goli la jioni kabisa la Najimu Magulu liliwahakishia maafande wa JKT Tanzania kuondoka na alama zote 3 dhidi ya wenyeji wao Mtibwa Sugar.
JKT walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 21 ya mchezo kupitia kwa Danny Reuben Lyanga, akiunganisha vizuri mpira wa adhabu uliochongwa vizuri na mabeki wa Mtibwa kuwa wazito kuzuia mpira huo uliommkuta mfungaji na kuitanguliza timu yake.
Dakika ya 44, Juma Nyangi Ganambali aliwasawazishia Mtibwa Sugar na kwenda mapumziko 1-1
Kipindi cha pili dakika ya 87, Najimu Magulu alipokea mpira uliodokolewa na Danny Lyanga na kupiga mpira wa chini uliommshinda Mohamed Makaka na kuendeleza msimu mbaya kwa Mtibwa Sugar.
JKT wanapata ushindi huo wakitoka kupoteza 1-0 nyumbani dhidi ya Dodoma Jiji. Wanafikisha alama 14, na kujiweka nafasi ya 6 huku Mtibwa Sugar wanaendelea kushika nafasia ya mwisho ya 16 kwenye msimao wakiwa na alama zao 5 baada ya michezo 9.