Msaada kwa Rasmus Hojlund! Man Utd wanataka mshambuliaji mpya mwezi Januari kusaidia usajili wa pauni milioni 72 na kubainisha walengwa watatu. Licha ya kufunga mabao matatu barani Ulaya, mshambuliaji huyo wa Denmark bado anasubiri kufungua akaunti yake ya mabao katika Ligi Kuu tangu ajiunge nayo kutoka Atalanta majira ya joto. Mashetani Wekundu sasa wanatafuta kusajili fowadi mwingine mwezi Januari ili kumsaidia chipukizi huyo, kwani wakuu wa klabu wanaamini Mdenmark huyo atakua zaidi ikiwa atacheza na kufanya mazoezi pamoja na mshambuliaji mwenye uzoefu. Majina ambayo yamependekezwa ni Ivan Toney wa Brentford, Mehedi Taremi wa Porto na Victor Osimhen wa Napoli.
Toney kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na kuondoka Brentford mwezi Januari huku vilabu vingi vinavyo cheza ligi ya nchini Uingereza (EPL) vikipigana vikumbo kumtaka fowadi huyo. Ndivyo ilivyokuwa kwa Osimhen ambaye mara kwa mara amekuwa akihusishwa na kuondoka Napoli baada ya msimu mzuri mwaka jana ambao aliisaidia klabu yake kuchukua taji la ligi kuu nchini Italia.