Boxing

PAMBANO LA FURY NA USYK LINAKUJA.

Rais wa juu wa masumbwi Duniani amesema Pambano la Tyson fury na Oleksandr Usyk lililokuwa kwenye hatihati ya kutofanyika litafanyika baada ya kuzungumza na pande zote mbili.

Published on

Bingwa wa masumbwi wa uzito wa juu Duniani (WBC) Tyson Furry, ambaye alikuwa na pambano mwisho wa wiki iliyopita dhidi ya Bingwa wa UFC, Francis Ngannou kwenye pambano la mizunguko 10 lisilo la ubingwa anategemewa kushuka ulingoni tena hivi karibuni kumkabili bondia kutoka nchini Ukraine, Oleksandr Usyk.

Awali pambano hilo lilipangwa kufanyika December 23 lakini kutokana na uzito wa pambano lililopita dhidi ya Ngannou, Fury alitangaza kuwa huenda pambano hilo likaahirishwa ili apate muda wa kutosha kupumzika.

Rais wa ngazi za juu Todd dyBoef amesema nguvu ya ziada imetumika kuwashawishi na tayari kila kitu kipo sawa,

Kazi kubwa inafanyika, Kazi nzito ya kuwafanya watu wakubaliane inafanywa. Sidhani kama pande zote zilihusishwa kuwa wapo tayari pambano kufanyika December, kila kitu kinaenda ndivyo sivyo.

Kwasasa tunaendelea kulishughulikia kuhusu tarehe na kila kitu. Nadhani kuna ahadi, kuna shauku kubwa ya pambano hili kufanyika.

Alisema Todd duBoef.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa Tyson Fury ni bora astaafu kuliko kucheza pambano na Usyk na mataji yake yote aachane nayo, Meneja waa Bondia huyo, Spencer Brown ameema huo ni uvumi usio na ukweli wowote.

Hilo halina ukweli wowote, hakuna kitu kama hicho, Tyson yupo tayari kupigana.

Spencer Brown, Meneja wa Tyson Fury.

Popular Posts

Exit mobile version