Fainali ya kwanza ya mashindano ya African Football League inatarajiwa kuanza kurindima hii leo kati ya Wydad Athletic Club ya Morocco dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Africa Kusini. Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu hizi mbili kukutana katika michuano hii mipya Barani Afrika iliyokuwa ikihusisha klabu nane kutika pande zote za Afrika, huku Afrika Mashariki ilikuwa ikiwakilishwa na klabu ya Simba.
Kuelekea katika mchezo huu mkubwa Barani Afrika, Mchezaji wa Wydad Athletic Club, Ayoub El Amloud amesema watafuata maelekezo ya kocha ambayo watapewa hii leo ili waweze kufanya vizuri.
Tunatoa salamu zetu za pole kwa familia ya kaka yetu Osama Filouh na mechi dhidi ya Mamelodi Sundowns haitakuwa rahisi.
Tumekutana na Mamelodi Sundowns kwenye mechi zaidi ya kumi (10), lakini kwasasa tutafata maelekezo ya kocha na tutafanya vizuri,
Mchezaji wa Wydad Athletic Club, Ayoub El Amloud.
Adil RAmzi kocha mkuu wa kikosi cha Wydad AC amesema huu ni mchezo wa mpira wa miguu, uko tofauti sana na mambo mengine.
Natoa salamu zangu za pole kwa familia ya Osama Falouh, mmoja kati yetu kwenye timu, ataendelea siku zote kuishi kwenye mioyo yetu, tutapambana ili kutimiza ndoto zake.
Ninajiamini na uwezo wa wachezaji wangu, hali ya hewa ni nzuri, mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns utakuwa wa tofauti sana. Utakuwa ni mchezo wa mpira wa miguu ni tofauti na mambo mengine.
Adil RAmzi kocha mkuu wa kikosi cha Wydad AC.
Mamelodi Sundowns kupitia kwa mchezaji wa kikosi hicho Marcelo Allende amesema wamejipanga kupambana ili kuimaliza meci ugenini kabla ya mchezo wa marejeano utakaopigwa Pretoria nchini Afrika Kusini.
Natuma salamu zangu za pole kwa kifo cha mchezaji wa Wydad AC. Mchezo hautakuwa rahisi lakini tutacheza ili tupate matokeo chanya kabla ya mechi ya marejeano itakayofanyika Pretoria.
Tunawajua vizuri Wydad AC na huu ni mchezo wa fainali, hautakuwa mchezo rahisi.
Marcelo Allende, Mchezaji wa Mamelodi Sundowns.
Rulani Mokwena kocha mkuu wa kikosi cha Mamelodi Sundowns anaamini kikosi chake kimejiandaa vyema kuelekea mchezo huo na maandalizi yote yamekamilika.
Tunahitaji kushughulika na umati wa mashabiki wa Wydad AC na tunahitajika mawazo yetu kuyaelekeza kwenye malengo yetu.
Tulikuja hapa msimu uliopita kucheza mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydad AC haukuwa mchezo rahisi kutikana na mashabiki wa Wydad walivyohudhuria kwa wingi.
Kuna michezo miwili, kwahiyo tunapaswa kuushughulikia mchezo wa kwanza vizuri ili turudi na matokeo mazuri kabla ya mchezo wa marejeano, tupo tayari, tumejiandaa na mchezo kwenye mazingira mazuri.
Rulani Mokwena, Kocha wa Mamelodi Sundowns.
Kwenye mchezo wa leo kutakuwa na muda wa ukimya kabla ya mchezo kuanza ili kuomboleza kifo cha mchezaji wa Wydad AC Osama Filouh aliyefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupaga ajali ya Gari.
Mchezo wa pili wa marejeano utapigwa katika dimba la Loftus Versfield, Pretoria, Afrika Kusini November 11.