NBC Premier League

KUELEKEA DERBY YA KARIAKOO LEO.

Siku nyingine ya burudani kwa wapenzi wa soka Nchini, kama sio ukanda huu wa Afrika Mashariki basi Afrika na pengine Dunia nzima. KARIAKOO DERBY.

Published on

Siku nyingine ya burudani kwa wapenzi wa soka Nchini, kama sio ukanda huu wa Afrika Mashariki basi Afrika na pengine Dunia nzima. KARIAKOO DERBY.

Simba v Yanga, inachagizwa utamu na mifumo inayofanana na aina ya uchezaji wa kufanana. 4-2-3-1 ndio mfumo mama kwa timu zote mbili na sioni kama kuna ambaye ataenda kucheza nje ya mfumo huo leo.

Vita kubwa kwenye Kiungo wote wakiwa na viungo watano. Watatu washambuliaji na wawili wakabaji ambao hawa tunawaita viungo wahimili na ndio hasa mfumo unawazunguka wao.

4-2-3-1 ni mfumo wa kisasa mbadala wa 4-4-2 Diamond, ikiua mshambuliaji mmoja na namba 10 kushuka chini kutengeneza umbo la viungo watatu na mara nyingi nafasi hii hucheza kiungo siku hizi sio mshambuliaji tena.

Wahimili wawili(Double Pivot),
Kwa timu zote mbili hutumia kiungo mmoja mkabaji na mwingine box to box amabaye anaongezeka wakati timu inashambulia huku kiungo mkabaji akibaki chini kuongeza idadi ya walinzi wanaobakia kuwa watatu kipindi hiki cha “Transition” ambapo hadi Walinzi wa pembeni wanakuwa wamepanda. Walimu wote wawili huingia na mbinu hii(Mudathir kama box to box, Aucho kama kiungo mlinzi kwa Yanga, Kanoute/Mzamiru kama box to box, Ngoma anabaki kama Kiungo mlinzi kwa Simba).

Uzuri wa mfumo huu pia ni namba kubwa wakati timu inashambuliwa pia, viungo watatu wa juu, hushuka chini kabisa na kumuacha namba 9 tu peke yake wakati timu haina mpira. Takribani wachezaji 9 wanakuwa nyuma ya mpira. Haishangazi kuonaga mechi ya wababe hawa huwa na magoli machache sana mara nyingi.

Nani atathubutu kubadili mfumo wake leo? Nani atataka kujaribu kitu kipya kwenye Derby ya Leo kwenye mazingira haya ya leo ya hali ya hewa ambayo sio rafiki sana kwa soka burudani?

Kitaalamu nimekupa mifumo mama yao na inacheza vipi. Mengine ni ya Walimu namna watakavyoamua kuingia leo. Yote kwa yote tunatarajia kuona mechi ya Ushindani na kila mtu anaihitaji.

KARIAKOO DERBY : A DERBY LIKE NO OTHER!

Popular Posts

Exit mobile version