Mchezo wa kwanza wa fainali ya michuano ya AFL umetamatika katika dimba la Mohamed V kwa mwenyeji Wydad AC kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Magoli ya Wydad AC yalifungwa na mlinzi wa Mamelodi Sundowns aliyejifunga mapema kipindi cha kwanza dakika ya 41 na kufanya mchezo huo uende mapumziko Wydad wakiwa kifua mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa kila timu ikitafuta matokeo yatakayowafanya wakae mahali salama, Mamelodi Sundowns wakapata Penati zakika ya 73 iliyopigwa na Abdelmounaim Boutouil dakika ya 73.
Dakika ya 78 Anas Serrhat akaipatia goli la uongozi klabu yake ya Wydad AC na hiyo kuwaweka katika hali ya ahueni kuelekea mchezo wa marejeano utakaopigwa nchini Afrika Kusini.
Katika mchezo huo Wydad AC wamepiga mashuti 8 langoni mwa Mamelodi Sundowns, mashuti matano (5) hayajalenga lango, mashuti mawili (2) yamelenga lango na moja (1) lilizuiliwa.
Mamelodi walipiga mashuti saba (7), Mashuti matatu (3) hayajalenga lango, mashuti mawili (2) yamelenga lango na mawili (2) yalizuiliwa.
- Wydad AC imepiga kona mbili (2), Mamelodi imepiga kona sita (6),
- Wydad AC imenaswa katika eneo la kuotea mara tatu (3) na Mamelodi Sundowns mara moja (1),
- Wydad wametengeneza nafasi za wazi 13, Mamelodi Sundowns imetengeneza nafasi 15.
- Wydad AC imepewa kadi za njano mbili (2) Mamelodi Sundowns haijapata.
Mchezo wa marejeano baina ya timu hizi mbili utapigwa November 11 katika dimba la Loftus Versfield, Pretoria, Afrika Kusini. Goli la ugenini linahesabika katika mashindano haya, kama Mamelodi Sundowns ikishinda goli moja pekee itatangazwa kuw bingwa wa mashindano haya.