Baada ya Simba kukubali kichapo cha goli 1-5 dhidi ya Yanga hapo jana hisia zilikuwa kubwa kwa mashabiki wa Simba, wengi walielekeza lawama zao kwa golikipa wa klabu hiyo Aishi Salum Manula wakidai kuwa nyota huyo amecheza mchezo huo akiwa bado hajarejea kwenye utimamu wake.
Manula amerejea kwenye kikosi cha kwanza cha Simba kwenye mchezo dhidi ya Yanga baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha yaliyokuwa yanamkabili.
Mchambuzi wa soka nchini Farham Kihamu amesema hakuna goli ambalo lilifungwa kwa uzembe wa golikipa huyo na magoli mengi yamefungwa kwa uwezo wa wafungaji.
Nimerudia tena magoli yote matano, sijaona hata goli moja la kumlaumu Aishi Manula pale kuwa kafanya uzembe kwa kifupi chuma zote zimepigwa kiustadi na zimetokana na uzembe wa wachezaji wa ndani.
Chuma ya kwanza Ngoma kapoteza mali sehemu hatarishi (karejee video), chuma ya pili Wachezaji wamejisahau kumsikilizia Mwamuzi, chuma ya tatu Putin kauza kibanda, chuma ya nne ni uzembe wa Mabeki na penati haina ufundi kwenye chuma ya tano.
Hakuna goli la kumlaumu Aishi hata moja pale sijaliona binafsi.
Farhan Kihamu, Ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.