EPL

GARNACHO AKWEPA ADHABU KISA EMOJI.

Nyota wa klabu ya Manchester United Alejandro Garnacho alifikishwa mbele ya kamati ya nidhamu kujieleza alimaanisha nini kutumia emoji mbili zenye rangi tofauti katika picha aliyopost akiwa na Andre Onana.

Published on

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Alejandro Garnacho amekwepa adhabu kutoka shirikisho la soka nchini England baada ya kupost picha akiwa na Andre Onana baada ya kuokoa mkwaju wa penalty dhidi ya Copenhagen kisha kwenye picha hiyo kuweka emoji za mikono miwili ikipiga tano yenye rangi nyeupe na nyeusi jambo ambalo lilitafsiriwa kuwa ni ubaguzi wa rangi.

Wengi waliamini huenda nyota huyo raia wa Argentina angekutana na adhabu kwa kosa hilo kama ilivyokuwa kwa nyota wa Manchester City Bernardo Silva ambaye alifungiwa mchezo mmoja mwaka 2019 kwa kupost katuni iliyotafsiriwa kuwa ubaguzi wa rangi kwa mchezaji mwenzake wa zamani wa klabu hiyo Benjamin Mendy.

Kamati ya nidhamu ya Wembley imetangaza kuwa Garnacho amepokea mara kadhaa jumbe za onyo kuhusu kile anachokiweka kwenye mitandao yake ya kijamii na hakuna hatua zinazochukuliwa.

Msemaji wa shirikisho la soka England (FA) amesema

Tumefanya uchunguzi kuhusiana na chapisho la Alejandro kwenye mtandao wake wa kijamii, tumemsikiliza pia mchezaji mawazo yake kama sehemu ya upelelezi wetu, na ameeleza kuwa matumizi ya emoji hizo mbili ni kuonyesha nguvu na uimara wa wachezaji wenzake, hasa hasa Harry Maguire na Andre Onana ambao walikuwa na wakati mzuri sana wakati wakiibuka na ushindi dhidi ya Copenhagen.

Tumeridhishwa na maelezo ya Alejandro Garnacho na kile alichokuwa anakimaanisha hivyo hatutaendelea na maswala ya kinidhamu tena.

Hata hivyo tumemkumbusha mchezaji kuhusu majukumu yake kwenye machapisho yake ya mitandao ya kijamii na matumizi ya emoji katika wakati ambao yataleta mafikirio tofauti.

Tutajadiliana pia na PFA kuhusu matumizi ya emoji na meseji vinavyofanana na elimu itolewe kuhusu hivi vitu.

Msemaji wa Shirikisho la soka England.

Andre Onana ametolea amemtetea pia nyota huyo Garnacho kwenye mtandao wake wa Instagram kwa kuandika,

Watu hawachagui namna gani naweza kuchukizwa, najua hasa Garnacho alikuwa ana maanisha nini, uwezo na nguvu, hili jambo halitakiwi kufika mbali.

Andre Onana kupitia mtandao wake wa Instagram.

Popular Posts

Exit mobile version