Top Story

CHAMA CHA SOKA UBUNGO KURUDIA UCHAGUZI.

Published on

November 7, 2023 chama cha soka wilaya ya Ubungo kilifanya mkutano katika ukumbi wa Rombo Green View uliyopo Wilaya ya Ubungo Jijini Dar Es Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa na Afisa Michezo wa Wilaya pamoja na wajumbe wa kamati yake wawili. Haya ni miongoni mwa yale yaliyojadiliwa katika mkutano huo;

  1. Mkutano mkuu wa UFA umejiridhisha kwamba wanachama waliofanya uchaguzi mnamo tarehe 4/11/2023 hawakuwa wanachama hai wa UFA na wametoka Wilaya zingine na picha zipo na wameomba kamati ya maadili walishughulikie hili hadi vyombo vya juu vya sheria.
  1. Mkutano mkuu wa UFA umeridhia kwa pamoja kujaza nafasi zote nne zilizo wazi na sio mbili ambazo DRFA wanazitaka kwa manufaa yao.
  2. Umoja wa klabu wameamua kwa pamoja na kuwapa maagizo viongozi ndani ya siku 90 waanze mchakato wa uchaguzi mbele ya viongozi wa BMT ngazi ya wilaya na msajili wa klabu ngazi ya wilaya.

Kwasasa Uchaguzi wa Wilaya ya Ubungo utasimamiwa na Kamati ya uchaguzi ya UFA na Sio Kamati nyingine kama ambavyo wajumbe wa mkutano huo walivyoadhimia kwa umoja wao. Nafasi zinatakazo fanyiwa uchaguzi ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, mjumbe DRFA pamoja na mjumbe wa zone.

Popular Posts

Exit mobile version