Ligi ya mabingwa Barani Afrika kwa upande wa Wanawake imeendelea jana kwa michezo miwili kuchezwa hapo jana katika uwanja wa Stade de san Pedro nchini Ivory Coast.
Mchezo wa mapema ulikuwa kati ya AS Mande kutoka Bamako Mali dhidi ya Ampem Darkoa ya Ghana mchezo uliomalizika kwa AS Mande kushinda 3-0.
Katika mchezo huo magoli yote matatu yalifungwa na Oumou Kone dakika ya 40′, 71′, 73 na hii ikawa hattrick ya kwanza ya mashindano haya ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika. Huu unakuwa ni ushindi wa kwanza wa AS Mande kushinda katika hatua ya Makundi baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Huracanes.
Mchezo mwingine uliopigwa hapo jana ulikuwa kati ya FAR Rabat ya Morocco dhidi ya Huracanes ya Equatoria Guinea mchezo uliomalizika kwa bingwa mtetezi FAR Rabat kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lililofungwa na Safa Banouk dakika ya 33.
MECHI ZIJAZO JUMAPILI ZA KUNDI B
23:00 AMPEM DARKOA vs HURACANES
23:00 AS MANDE vs FAR RABAT
Ligi ya mabingwa Barani Afrika kwa upande wa wanawake inatarajiwa kuendelea tena kesho kwa michezo ya Kundi A.
23:00 SPORTING CASABLANCA vs JKT QUEENS
23:00 MAMELODI SUNDOWNS LADIES vs ATHLETICO ABIDJAN